Mawazo makuu
Hali ya fedha
Finance inaonyesha Assets, yaani mali; Liabilities, yaani madeni; na Equity, kinachobaki. Balance check iwe Balanced; isipolingana, chunguza kwanza kabla ya kuendelea. Finance inafunguliwa na mmiliki, msimamizi na meneja wa tawi.
Fuatilia mkopo kwenye Transactions
Kwenye Transactions, tafuta kwa namba ya mkopo; miamala hubeba kumbukumbu za ndani za Adili, si namba ya mobile money. Kila rejesho linaingia pande mbili: deni la mkopo linapungua na fedha zinaingia kwenye till, kwa mfano wetu Head Office Till, huku riba ikihesabiwa kama mapato.
Rekebisha kwa journal
Kurekebisha vitabu, chagua New journal kwenye Journals: debit akaunti moja na credit nyingine kwa kiasi hicho hicho ili isomeke Balanced, kisha Save draft na Submit for approval, yaani iwasilishe kwa idhini. Mtu wa pili ndiye anaidhinisha; huwezi kuidhinisha journal yako mwenyewe. Ikishawekwa haifutwi; Reverse hutengeneza marekebisho yanayohitaji idhini pia.
Credit Wallet
Credit Wallet, chini ya Settings, hulipia SMS za vikumbusho na ripoti za mikopo; ongeza salio likipungua. Weka tahadhari ya barua pepe, kwa mfano wetu shilingi elfu ishirini, ili timu ijue mapema. Mikopo yenyewe hutolewa kutoka akaunti za fedha kama till, si kutoka Credit Wallet.