Fedha na uzingatiaji ยท Somo 13 kati ya 15

Ulinganishaji wa akaunti za benki

Pakia taarifa ya benki au wallet, oanisha safu zake, linganisha, na eleza mstari ambao Adili haiwezi kuulinganisha.

Takriban dakika 12

Mawazo makuu

1

Anza na taarifa

Hapa unalinganisha taarifa yako na Adili, mstari kwa mstari. Chagua New reconciliation, taja chanzo, kwa mfano wetu Head Office Till, kisha chagua faili la taarifa: CSV au Excel kutoka benki au wallet.

2

Oanisha safu

Adili inasoma safu kutoka vichwa vya faili. Kila mstari unahitaji tarehe na kiasi; mwelekeo hutofautisha fedha zinazoingia na zinazotoka, na kumbukumbu hufanya ulinganisho uwe wa uhakika. Bila mwelekeo, mistari huzuiliwa badala ya kubahatishwa, mpaka uingize taarifa upya ukiwa umeoanisha safu ya debit/credit.

3

Linganisha na kagua jozi

Ingiza mistari, kisha Run matching, yaani linganisha, na ukague kumbukumbu, kiasi na mwelekeo kwa kila jozi; kwa mfano wetu mistari minne kati ya mitano ililingana, na utoaji wa mkopo ulilingana kwa kumbukumbu yake. Utoaji hulinganishwa kwa fedha iliyotoka kweli baada ya ada iliyokatwa: 980,000 kwa mkopo wa 1,000,000.

4

Eleza tofauti, kisha Finish

Mstari usio na muamala kwenye Adili, kama ada ya benki ya 5,000 (BANK-FEE-10), unabaki bila kulingana. Iandike ada hiyo kwenye vitabu vyako ili hesabu zilingane, na ubonyeze Finish kila mstari ukishalingana au kuelezwa.

Mazoezi

Jaribu kwenye taasisi yako ya mafunzo

  1. 1. Pakua taarifa ya CSV au Excel ya akaunti ya fedha kutoka benki au wallet, au tengeneza ndogo ya mafunzo yenye kumbukumbu za utoaji na rejesho la mafunzo na mstari mmoja wa ada ya benki.
  2. 2. Fungua Reconciliation, chagua New reconciliation, andika akaunti kwenye Bank or source name (kwa mfano wetu Head Office Till) na uambatishe taarifa.
  3. 3. Chagua Map columns na uhakikishe Transaction date, Amount, Debit / credit na Reference / transaction ID zimeoanishwa.
  4. 4. Chagua Import (kitufe kinaonyesha idadi ya mistari yako, kama Import 5 rows), kisha Run matching.
  5. 5. Kagua kumbukumbu, kiasi na mwelekeo kwa kila jozi iliyolingana, na uandike kwa nini mstari usiolingana hauna muamala kwenye Adili.
  6. 6. Andika ada yoyote ya benki kwenye vitabu vyako, kisha bonyeza Finish kila mstari ukishalingana au kuelezwa.

Jipime

Tazama video na ufanye jaribio

Ingia ili kutazama video ya somo hili, kujibu maswali yake 4 na kulihesabu kwenye cheti chako. Maendeleo yako yanahifadhiwa.

Fungua kwenye mafunzo yangu